HII BLOGI NI MAALUM KWA AJILI YA KUWAFAHAMISHA WATU WOTE NJIA YA KWELI YA KWENDA MBINGUNI/PEPONI. NJIA HIYO NI YESU KRISTO PEKEE. WALIOMWAMINI WOTE NI WALIOBATIZWA KATIKA MAJI MENGI, WAMEOKOKA NA KUJAZWA/KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU NA NENO LA KWELI.
Search This Blog
Thursday, December 27, 2012
SEMINA YA KRISMAS 2012 NA SAID SHABAN KATIKA KANISA LA PENTEKOSTE TZ, BAGAMOYO
SOMO KUU: MADHARA YA USENGENYAJI NA UZUSHI NDANI YA KANISA LA KRISTO
Katika semina hii ambayo ilidumu kwa muda wa siku tatu (tarehe 23-25/12/2012), Mtumishi wa Mungu, Ndugu Eliya Shabani, ambaye anaishi Kibaha, alionya sana kanisa la Kristo juu ya kujiepusha na usengenyaji na uzushi kwani atendaye mambo hayo hana tofauti na mchawi au muuaji na jambazi.
Aliongeza kuwa, kanisa la nyakati za sasa linashindwa kudhihirisha ukuu, uweza na mamlaka ya Mungu wa Kweli, Muumbaji kutokana na waumini wake wengi kujichanganya katika mambo ya usengenyaji na uzushi ambavyo vinaondoa uwepo wa Roho mtakatifu ndani ya mkristo na kanisa la Mungu kwa ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment